*lackstar tours and safaris.*
Mwanafunzi wa Darasa la tatu shule ya Msingi Ikelu Makambako mkoani Njombe, Claud Frolence (9) amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kikoi akiwa anacheza na wenzake shambani.
Mwanafunzi wa Darasa la tatu shule ya Msingi Ikelu Makambako mkoani Njombe, Claud Frolence (9) amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kikoi akiwa anacheza na wenzake shambani.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Hamisi Issa amesema mwanafunzi huyo alikwenda shambani na wazazi wake na wadogo zake watatu akiwa huko walinza kucheza na wadogo zake na baadae kuchukua kikoi na kuanza kucheza michezo ya kujaribu namna ya kujinyonga.
Aidha kamanda Kamanda Issa amewataka wazazi kuwa makini na malezi ya watoto wao kwani malezi ya Watoto ni pamoja na kuangalia aina ya michezo wanayoicheza na katika mazingira yanayofaa.
Comments
Post a Comment