Chama cha CHADEMA kimesema hakitashiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Muhambwe lililopo Wilayani Kibondo Mkoa wa Kigoma.
Jimbo la Muhambwe liko wazi baada ya aliyekuwa Mbunge Atashasta Nditiye kufariki dunia Februari 12, 2021 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa mkoani Dodoma alikokuwa akipatiwa matibabu.
Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Benson Kigaila amesema baada ya kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika March 31, 2021 kwa njia ya mtandao wameazimia kutoshiriki uchaguzi huo kutokana na mazingira ya tume ya uchaguzi kutotenda haki.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeshatangaza kuwa uchaguzi katika jimbo hilo utafanyika May 2, 2021.
Comments
Post a Comment