Skip to main content

Mfahamu Jonas Savimbi kiundani zaidi

*lackstar tours and safaris.*


 


Februari 22, 2002 vyombo vingi vya habari duniani kote vilitawaliwa na habari kubwa ya kuuawa kwa mfalme wa pori na mwanaume aliyeisumbua serikali ya Angola kwa zaidi ya miaka 27 akiongoza vita vya msituni dhidi ya vikosi vya serikali.

Jonas Malheiro Savimbi, alikuwa mtoto wa pekee kwa baba yake Lote, aliyekuwa mfanyakazi wa reli ya Benguela na mhubiri wa kanisa la Protestanti lililokuwa likifadhiliwa na Wamarekani.

Pamoja na baba yake kuwa muumini wa dini kamwe Jonas hakuwa muumini, tangu utoto wake alikuwa mtukutu.

Alisoma katika shule za Kiprotestanti na Kikatoliki, lakini akiwa na miaka 24 alipata udhamini wa kwenda kusoma Ureno ambapo alimalizia masomo yake ya sekondari na somo la lazima la siasa huku akishindwa kuanza kwa wakati masomo ya udaktari wa binadamu aliyotakiwa kuyachukua.

Mwaka 1966 alianzisha vuguvugu la Unita kama harakati ya kukomboa Angola kutoka ukoloni wa Ureno.

Katika nyakati zake za awali, kabla ya kuanzisha Unita, alijiunga na chama cha wapigania uhuru wa MPLA mwaka 1964, muda mfupi baadaye alijiunga na chama cha FNLA.

Mwaka huohuo alipata fursa ya kufanya ziara maalumu China na aliahidiwa kupatiwa nafasi zaidi kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi na misaada ya zana za kijeshi.

Hatua hiyo ilitokana na mgongano wa kimasilahi, baada ya FNLA na MPLA kuanza kupingana kuhusu nani anastahili kupewa nchi iwapo watapata uhuru, hivyo muda mfupi baadaye wakoloni hao walitoa taarifa kueleza kwamba Savimbi anapigana kwa ajili ya masilahi yao.

Hatua hiyo ilisababisha kuungwa mkono na Marekani iliyokuwa na masilahi tofauti na MPLA iliyoungwa mkono na Wasovieti tangu mwaka 1974 na kilijipambanua kufuata mrengo wa Marxist-Leninst kuanzia mwaka 1977, wakati Savimbi alijipambanua kufuata sera za Mao na kuungwa mkono na China.

Vita baina ya MPLA na Unita hata hivyo ilikuwa na sababu nyingi za ndani na kwa hiyo kuanza kutumiwa kama chanzo cha mvutano wakati wa vita baridi baina ya Marekani na USSR.


Mwaka 1966 baada ya kurejea kutoka nchini China ambako alienda kupata mafunzo ya kijeshi alirudi na kuunda UNITA na kuanza kupambana na serikali ya kikoloni sambamba na vyama vingine ambavyo vyote vilikuwa vikipigana kumtoa mreno.

Hapa ndipo jina la Jonas Savimbi likaanza kusikika kote duniani kutokana na mbinu kubwa za kijeshi alizonazo huku akisapotiwa na wananchi kutoka kabila lake la Bieno.

Huku akipata sapoti kubwa kutoka China na baadaye Marekani, aliongoza vita vikali kwa muda wa miaka zaidi ya 20 huku akiwa ni tishio kubwa kwa Serikali ya Luanda. Kuna muda aliwahi karibia kuipindua serikali ya Rais Dos Santos.

Akiwa na uwezo wa kuzungumza lugha saba kiufasaha zikiwemo tatu za ndani ya bara la Afrika na nne nje ya bara aliweza kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali kuwaomba msaada wa zana za kivita na alifanikiwa kuwa na jeshi imara.

Aliwahi kunusurika kuuawa mara kadhaa likiwemo jaribio la Februari 1990 ambapo aliponea chupuchupu na kukimbilia nchini Marekani na kufanikiwa kuonana na Rais Bush ambaye alimuahidi kumuongezea zana zaidi za kijeshi na baada ya kupona alirejea nchini Angola kuendeleza mapambano.

Baada ya kunusurika kuuawa zaidi ya mara 20 na vikosi vya serikali ya Angola huku taarifa za kuuawa kwake zikiripotiwa zaidi ya mara 15 hatimaye 22 Februari 2002 Jonas Savimbi aliuawa.

Maauaji yake yalitokea kwenye mapigano baina ya vikosi vyake dhidi ya serikali kwenye mto uliopo jimbo la Moxico eneo ambalo alizaliwa. Mapigano hayo ya kushtukiza yalipangwa baada ya vibaraka kutoa siri za mahali alipo Savimbi na baadhi ya wasaidizi wake muhimu, haikuwa kazi rahisi kumuua.

Aligundulika alipo kuwa amejificha baada ya kufanya kosa la kutumia satellite phone na huo ndio ukawa mwisho wake. Osama alikuwa hafanyi kosa kama hilo,ndio maana ilikuwa vigumu kubaini alikuokuwa amejichimbia.

Kwenye shambulio hilo kali kuwahi kufanywa na vikosi vya serikali dhidi ya kikosi cha Savimbi walifanikiwa kumpiga risasi 15 mwilini mwake, alipigwa kichwani, kifuani na sehemu za miguuni na aliweza kumudu na kuendeleza mapambano kwa zaidi ya saa nne kabla ya kuishiwa damu na kuanguka chini na kufariki.

Tukio la kuuawa kwake bado limeacha maswali mengi mpaka leo inakuwaje na aliwezaje kuhimili kuendeleza mapambano hata baada ya kupigwa risasi 15 mwilini mwake?

Alizikwa kwenye makaburi ya nyumbani kwao ya Luena na kuhudhuriwa na wapiganaji mbalimbali wa UNITA.

Mauaji yake yalimaanisha mwisho wa mapigano ya msituni nchini Angola, Chuma kilikuwa kimeangushwa, wasaidizi wake hawakuwa na mbinu na uwezo kama Savimbi.

Baada ya kifo chake serikali kuu ilitangaza ya kwamba hatimaye wameangusha mbuyu wa chuma uliowasumbua miaka mingi.

Wapo wanaoamini mpaka kesho kwamba Jonas Savimbi hakuwa binadamu wa kawaida, walimuona ni binadamu wa pekee mwenye uwezo mkubwa kuliko binadamu wa kawaida.

Wenye imani potofu walimfananisha na jini au mzimu unaotembea popote na wakati wowote bila kujali hatari iliyo mbele yake.

Hadi mauti yake yanamkuta ameacha watoto na wake wengi ambao idadi yake haijawekwa wazi kulingana na sehemu kubwa ya maisha yake alikuwa akiishi msituni.

Ndivyo ilivyokuwa kwa Jonas Savimbi ambaye kitendo chake cha kugomea kurudiwa kwa uchaguzi wa rais wa nchi hiyo na kuamua kuingia msituni kulipelekea kuuawa kwake.

Savimbi alifanya kosa moja kubwa alilazimisha vikosi vyake kuingia msituni kupambana na serikali akiwa bado hajajipanga vyema, ni bora angekubali kurudia uchaguzi dhidi ya Rais Dos Santos.

Bahati mbaya hakulikumbuka hilo, aliwaza jambo moja tu kuingia msituni kuandaa kikosi chake tayari kuuondoa utawala wa Dos Santos.

Aliingia msituni kipindi ambacho tayari kikosi chake kilikuwa kimeingiliwa na vibaraka ‘spy’ kutoka ndani ya kabila lake, vibaraka hawa waliandaliwa kwa ustadi mkubwa na ndiyo walihusika kutoa siri zote za nini kilikuwa kinaendelea kwenye kikosi cha Savimbi.

Comments

Popular posts from this blog

8 Most Beautiful Brazilian Actresses

#subscribe on youtube "YOHANEC CHANG'A" Na Yohanec Chang'a- Iringa Brazilian women are like the sun: bright, positive, and so dang hot. It’s especially evident when you look at the models, actresses, and other juicy celebs. These women have used their immense sexuality and became the standard of beauty for men around the world. Here are the eight most beautiful Brazilian actresses. 1. Vivianne Pasmanter Vivianne’s parents dreamed that their daughter would do ballet professionally, but the girl did not like that idea and instead wished to become an actress. And she did it. Now Pasmanter can, without exaggeration, be called one of the most famous actresses on Brazilian TV series such as “Nuovo Mundo” and “Alén, Luz de Luna.” 2. Christine Fernandes Although Christine was born in Chicago, Illinois, the future actress returned to her parents’ historical homeland in Brazil at the age of three. She came to the film industry from the modeling business and almost immediately s...

HAPPY BIRTHDAY BABA ASKOFU

#subscribe on youtube "YOHANEC CHANG'A" Heri ya kumbukizi ya siku mfanano ya kuzaliwa kwako Mhashamu Askofu Method Kilaini, Askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba. Wapendwa karibuni tuungane na kumtakia heri na matashi mema Baba Askofu Kilaini anapofanya kumbukizi ya siku mfanano ya kuzaliwa.

PETER MSECHU NATAKA NIONGEE NA WEWE KAKA KUHUSU TUNGO ZAKO KWA HAYATI MAGUFULI

#subscribe on youtube "YOHANEC CHANG'A" WAKATI bado tunaomboleza msiba mzito wa Taifa wa kuondokewa na Mpendwa wetu, Aliyekuwa Rais wa Taifa letu la Tanzania, Mpenda Amani, Mpenda watu wake hususani wale wenye hadhi ya chini na kipato kidogo, Mpenda Maendeleo, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Kaka Peter Msechu naomba niongee na wewe kitu katika Tasnia yako ya Muziki... Kiukweli baada ya kutangazwa Kifo cha Hayati Dkt. Magufuli Machi 17, 2021 na Aliyekuwa Makamu wa Rais kipindi hicho, Mama Samia Suluhu Hassan, Wasanii wengi nchini walijitokeza kutunga tungo (Nyimbo) mbalimbali kumuenzi Mpendwa wetu aliyetangulia mbele ya haki. Tumeona tungo nyingi zilizojaa wasifu wakumuenzi Hayati Dkt Magufuli, tungo hizo kutoka kwa Wasanii hao wa Tanzania na Vikundi mbalimbali vya Muziki ziliwavutia watu wengi kutokana na kubeba ujumbe wa kweli kwa Taifa letu. Tumeona vikundi kama Tanzania One Theatre (TOT), Vikundi kutoka Makanisa mbalimbali nchini na Wasanii wa Muziki wa kizazi ...