HABARI, JAMII,
* Kifo cha Rais Magufuli chawaumiza na kuwaliza watanzania, wanaAfrika na ulimwengu kwa ujumla.
Na Mwandishi wetu Globu ya Jamii
TULIKUPENDA, Tunakupenda na yote uliyofanya kwa nchi yetu vitaishi mioyoni mwetu, ni kauli za watanzania wengi baada ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Magufuli aliyefariki dunia jana katika hospitali ya Mzena Mkoani Dar es Salaam alipokuwa akitibiwa maradhi ya moyo.
Rais Magufuli (61,) anaingia katika orodha ya viongozi wakuu wa nchi barani Afrika waliofariki wakiwa madarakani, Magufuli ameongoza kwa kuwa kipindi cha 2015/ hadi Machi 2021, Marais wengine ni pamoja na;
Pierre Nkurunziza (64)
Alikua Rais wa nane wa Burundi na alihudumu kwa miaka 15 (Januari hadi Juni 2020) na alifariki dunia 2020 kwa mshtuko wa moyo.
Michael Sata (77)
Alikua Rais wa Zambia aliyehudumu kama Waziri kwa miaka ya 1990's kabla ya kuongoza taifa hilo kuanzia 2011 na alifariki dunia 2014 kwa maradhi ambayo hayakutajwa.
Meles Zenawi (57)
Alikuwa Waziri Mkuu wa pili wa Ethiopia kabla ya kupata nafasi ya kiti cha urais na alifariki dunia 2012 nchini Ubelgiji kwa maradhi ambayo hayakutajwa.
John Atta Mills (68,)
Alikuwa Rais wa Ghana kuanzia 2009 hadi 2012, awali alikuwa makamu wa Rais katika kipindi cha 1997 hadi 2001 na alifariki dunia 2012 kwa maradhi ya saratani ya koo/ kiharusi.
Bingu wa Mutharika (78)
Alikua wa Rais wa tano wa Malawi na kuhudumu kwa kipindi cha 2004 hadi Aprili 2012 alipofariki dunia kwa mshtuko wa moyo.
Malam B. Sanha (64)
Alikuwa Rais wa Guinea. Bissau aliyehudumu kwa kipindi cha 2009 hadi 2012 na alifariki dunia Januari 9, 2012 nchini Ufaransa kwa maradhi ya kisukari.
Mu'ammar Gaddafi (69)
Afahamika zaidi kama Colonel Gadafi, Mwanamapinduzi wa Taifa la Libya alikuwa Rais wa Libya kuanzia 1977/ 2011 na alifariki dunia 2011 kwa kuuwawa na waasi.
Umaru M. Yar'Adua (58)
Alikua Rais wa Nigeria kuanzia 2007 hadi 2010 na alifariki mwaka 2010 kwa matatizo ya moyo.
Mfalme Hassan 11 (70)
Alikuwa mfalme wa Morocco alifariki 1999 kwa homa ya mapafu.
Ibrahim B. Mainassara (50)
Alikua mwanajeshi na Rais wa Niger na alifariki dunia 1999 kwa kuuawa.
Laurent D. Kabila (61)
Alikua Rais wa tatu wa Congo DRC alishiriki kwa karibu katika kumungo'oa Mobutu Seseseko na alifariki dunia Januari 16, 2001 kwa kuuawa.
Muhammad H.I Egal (73)
Alikua Rais wa Somalia na kabla ya kushika wadhifa huo alikuwa waziri mkuu na alifariki dunia 2002 kwa maradhi ambayo hayakutajwa.
Levy Mwanawasa (59)
Alikuwa Rais wa tatu wa Zambia kuanzia 2002 hadi 2008 na alifariki duniani 2008 kwa maradhi ya kiharusi.
Lansana Conte (74)
Alikua Rais wa pili wa Guinea kutoka kabila la Susu na alifariki dunia 2008 kwa maradhi ya kisukari/ugonjwa ya moyo.
Comments
Post a Comment