Skip to main content

LOWASSA AMLILIA DKT. MAGUFULI

#subscribe on youtube "YOHANEC CHANG'A"

Salamu za rambirambi.

Bwana Yesu Asifiwe,
Tumsifu Yesu Kristo,
Salaam Aleikum...
MOYO wangu umeugua baada ya kupata taarifa za kifo cha mpendwa wetu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli kilichotokea Jumatano ya wiki hii, Machi 17, 2021.

Naomba nichukue fursa hii kutoa POLE zangu kwa mjane wa Rais, Mama Janeth Magufuli, wana familia, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote.

Kifo cha Rais Magufuli niliyemfahamu kwa miaka mingi tangu alipoingia bungeni mwaka 1995 na baadaye tukahudumu wote katika serikali ya marehemu Rais Benjamin Mkapa ni pigo kubwa kwa taifa.

Ninakumbuka namna nilivyofanya naye kazi vizuri na kwa ukaribu na kwa ushirikiano mkubwa wakati Rais Jakaya Kikwete aliponiteua kuwa Waziri Mkuu mwaka 2005.

Mwaka 2015, wote tukiwa wagombea tulishindana kwenye kinyan’ganyiro cha Urais, nilimuona ni mtu mwenye maono na moyo mwema wa kutaka kuliongoza taifa hili, mtu mwenye uthubutu wa kutaka matokeo na Tanzania mpya.

Natambua na kuheshimu uchapakazi wake na namna alivyoweza kurudisha nidhamu ya watumishi wa Serikali na ujasiri wake katika ujenzi wa miradi mikubwa ya miundombinu.

Ni wazi kifo cha Rais Magufuli kilichotokea takriban miezi minne tu tangu aingie madarakani katika muhula wake wa pili wa urais kimeliacha taifa katika simanzi kubwa kwa kumpoteza kiongozi shupavu, mzalendo wa kweli, mtetezi wa wanyonge na mchapakazi hodari asiyechoka.

Nitumie fursa kuwaomba Watanzania wenzangu kusimama pamoja na kuliombea taifa amani, umoja na mshikamano wa dhati wakati wote wa kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya kumpoteza jemedari wetu Rais Magufuli.

Si jambo rahisi kwa nchi kumpoteza kiongozi wake mkuu wakati akiwa madarakani.

Kwa sababu hiyo tunapaswa kusimama pamoja na Rais Mama Samia Suluhu Hassan na kumuombea aweze kusimama imara na kuliongoza taifa kwa weledi na hatimaye kutuvusha salama.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina lake Lihimidiwe!
Edward Ngoyai Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu

Comments

Popular posts from this blog

8 Most Beautiful Brazilian Actresses

#subscribe on youtube "YOHANEC CHANG'A" Na Yohanec Chang'a- Iringa Brazilian women are like the sun: bright, positive, and so dang hot. It’s especially evident when you look at the models, actresses, and other juicy celebs. These women have used their immense sexuality and became the standard of beauty for men around the world. Here are the eight most beautiful Brazilian actresses. 1. Vivianne Pasmanter Vivianne’s parents dreamed that their daughter would do ballet professionally, but the girl did not like that idea and instead wished to become an actress. And she did it. Now Pasmanter can, without exaggeration, be called one of the most famous actresses on Brazilian TV series such as “Nuovo Mundo” and “Alén, Luz de Luna.” 2. Christine Fernandes Although Christine was born in Chicago, Illinois, the future actress returned to her parents’ historical homeland in Brazil at the age of three. She came to the film industry from the modeling business and almost immediately s

HAPPY BIRTHDAY BABA ASKOFU

#subscribe on youtube "YOHANEC CHANG'A" Heri ya kumbukizi ya siku mfanano ya kuzaliwa kwako Mhashamu Askofu Method Kilaini, Askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba. Wapendwa karibuni tuungane na kumtakia heri na matashi mema Baba Askofu Kilaini anapofanya kumbukizi ya siku mfanano ya kuzaliwa.

PETER MSECHU NATAKA NIONGEE NA WEWE KAKA KUHUSU TUNGO ZAKO KWA HAYATI MAGUFULI

#subscribe on youtube "YOHANEC CHANG'A" WAKATI bado tunaomboleza msiba mzito wa Taifa wa kuondokewa na Mpendwa wetu, Aliyekuwa Rais wa Taifa letu la Tanzania, Mpenda Amani, Mpenda watu wake hususani wale wenye hadhi ya chini na kipato kidogo, Mpenda Maendeleo, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Kaka Peter Msechu naomba niongee na wewe kitu katika Tasnia yako ya Muziki... Kiukweli baada ya kutangazwa Kifo cha Hayati Dkt. Magufuli Machi 17, 2021 na Aliyekuwa Makamu wa Rais kipindi hicho, Mama Samia Suluhu Hassan, Wasanii wengi nchini walijitokeza kutunga tungo (Nyimbo) mbalimbali kumuenzi Mpendwa wetu aliyetangulia mbele ya haki. Tumeona tungo nyingi zilizojaa wasifu wakumuenzi Hayati Dkt Magufuli, tungo hizo kutoka kwa Wasanii hao wa Tanzania na Vikundi mbalimbali vya Muziki ziliwavutia watu wengi kutokana na kubeba ujumbe wa kweli kwa Taifa letu. Tumeona vikundi kama Tanzania One Theatre (TOT), Vikundi kutoka Makanisa mbalimbali nchini na Wasanii wa Muziki wa kizazi