#subscribe on youtube "YOHANEC CHANG'A"
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Machi 28,2021, imetoa angalizo la uwepo wa mvua kubwa kwa siku mbili kuanzia kesho Machi 29 na 30 mwaka huu katika mikoa
Katika taarifa iliyotolewa na TMA imeonyesha mvua hiyo yenye uwezekano wa wastani, itanyesha kesho Machi 29, kwenye baadhi ya maeneo ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani inayojumlisha Visiwa vya Mafia, Lindi, na Morogoro pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Aidha mvua hiyo inatarajiwa kunyesha kesho, Machi 30, kwenye baadhi ya maeneo ya mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, shinyanga, Kigoma, Katavi, Tabora, Rukwa, Mbeya, Songwe, Njombe, Ruvuma pamoja na kusini mwa mkoa wa Morogoro.
Athari zinazoweza kujitokeza ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji jambo linaloweza kuathiri shughuli za kiuchumi na ucheleweshwaji wa usafiri. Hata hivyo, TMA imewataka wananchi kuzingatia angalizo hilo.
Taarifa hiyo inayoelezea hali ya hewa kwa siku nne kuanzia Machi 29 imeonesha kuwepo kwa hali ya kawaida ya hewa kwa siku ya Machi 31 na Aprili Mosi, 2021.
Comments
Post a Comment