Skip to main content

NEC YATANGAZA UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE JIMBO LA MUHAMBWE, KIGOMA

#subscribe on youtube "YOHANEC CHANG'A"
Lackstar tours and safaris.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Willson Mahera

 Na Mwandishi Maalum, Dodoma

TUME ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza Ratiba ya uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Jimbo la Muhambwe, mkoani Kigoma baada ya kupokea Barua kutoka kwa Spika wa Bunge kuwa kiti hicho kiko wazi.

Taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya habari Jijini Dodoma leo, 27 Machi, 2021, na kusainiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Willson Mahera amesema uchaguzi huo umeapangwa kufanyika tarehe 2 Mei,2021.

“Tume ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye kwa kuzingatia kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, ameitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi ya kiti cha Ubunge katika Jimbo la Muhambwe, Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Mkoani Kigoma,” alisema Dkt Mahera.

 

Aidha, kwa kuzingatia kifungu cha 37 (1) (b), cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, sura ya 343 ambacho kinaitaka Tume kujaza nafasi ya kiti cha Ubunge katika kipindi kisichopungua siku 20 na kisichozidi siku 50 tangu kutokea kwa sababu iliyoacha nafasi wazi ya kiti hicho.

“Kutokana na matakwa hayo ya kisheria, Tume inautaarifu Umma kuwa Jimbo la Muhambwe liko wazi na uteuzi wa wagombea utafanyika tarehe 3 Aprili, 2021 Hivyo, uchaguzi ambayo ni siku ya 49 tangu kutokea kwa kifo hicho,”alisema Dkt. Mahera.

Alisema kuwa maandalizi kwaajili ya uchaguzi huo yameshafanyika na kazi ya utoaji fomu za uchaguzi kwa wagombea inaanza 28 Machi hadi 3 Aprili, 2021 huku uteuzi wa wagombea watakao wania nafasi hiyo ukifanyika  3 Aprili mwaka huu.

Aidha Dkt Mahera amesema kampeni za uchaguzi katika jimbo hilo zitaanza 3 Aprili 2021 na zitafikia ukomo wake Mei mosi mwaka huu na uchaguzi kufanyika 2 Mei,2021.

Mahera alisema yayari Tume imekwisha vitaarifu Vyama vya Siasa kwa njia ya barua juu ya kuwepo kqwa uchaguzi huo mdogo na inavikumbusha kuzingatia sharia, kanuni, Maadili ya Uchaguzi, Miongozo na Maelekezo ya Tume wakati wote wa kipindi cha Uchaguzi.

Pia Mahera alitumia fursa hiyo kutoa salamu za pole kwa viongozi wa Serikali, Familia na Watanzania wote kufuatia kifo cha  aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt John Pombe Magufuli.

 “Tume inatoa pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Familia ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, Chama cha Mapinduzi na watanzania wote kwa ujumla,” alisema Dkt Mahera.

Uchaguzi katika jimbo la Muhambwe unafanyika baada ya Mbunge wa Muhambwe (CCM) mkoani Kigoma Atashasta Justus Nditiye kufariki dunia Februari 12, 2021 ambaye alifariki akiwa Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kupata ajali ya gari eneo la Name name jijini humo Februari 11, 2021.

Comments

Popular posts from this blog

8 Most Beautiful Brazilian Actresses

#subscribe on youtube "YOHANEC CHANG'A" Na Yohanec Chang'a- Iringa Brazilian women are like the sun: bright, positive, and so dang hot. It’s especially evident when you look at the models, actresses, and other juicy celebs. These women have used their immense sexuality and became the standard of beauty for men around the world. Here are the eight most beautiful Brazilian actresses. 1. Vivianne Pasmanter Vivianne’s parents dreamed that their daughter would do ballet professionally, but the girl did not like that idea and instead wished to become an actress. And she did it. Now Pasmanter can, without exaggeration, be called one of the most famous actresses on Brazilian TV series such as “Nuovo Mundo” and “Alén, Luz de Luna.” 2. Christine Fernandes Although Christine was born in Chicago, Illinois, the future actress returned to her parents’ historical homeland in Brazil at the age of three. She came to the film industry from the modeling business and almost immediately s...

HAPPY BIRTHDAY BABA ASKOFU

#subscribe on youtube "YOHANEC CHANG'A" Heri ya kumbukizi ya siku mfanano ya kuzaliwa kwako Mhashamu Askofu Method Kilaini, Askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba. Wapendwa karibuni tuungane na kumtakia heri na matashi mema Baba Askofu Kilaini anapofanya kumbukizi ya siku mfanano ya kuzaliwa.

PETER MSECHU NATAKA NIONGEE NA WEWE KAKA KUHUSU TUNGO ZAKO KWA HAYATI MAGUFULI

#subscribe on youtube "YOHANEC CHANG'A" WAKATI bado tunaomboleza msiba mzito wa Taifa wa kuondokewa na Mpendwa wetu, Aliyekuwa Rais wa Taifa letu la Tanzania, Mpenda Amani, Mpenda watu wake hususani wale wenye hadhi ya chini na kipato kidogo, Mpenda Maendeleo, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Kaka Peter Msechu naomba niongee na wewe kitu katika Tasnia yako ya Muziki... Kiukweli baada ya kutangazwa Kifo cha Hayati Dkt. Magufuli Machi 17, 2021 na Aliyekuwa Makamu wa Rais kipindi hicho, Mama Samia Suluhu Hassan, Wasanii wengi nchini walijitokeza kutunga tungo (Nyimbo) mbalimbali kumuenzi Mpendwa wetu aliyetangulia mbele ya haki. Tumeona tungo nyingi zilizojaa wasifu wakumuenzi Hayati Dkt Magufuli, tungo hizo kutoka kwa Wasanii hao wa Tanzania na Vikundi mbalimbali vya Muziki ziliwavutia watu wengi kutokana na kubeba ujumbe wa kweli kwa Taifa letu. Tumeona vikundi kama Tanzania One Theatre (TOT), Vikundi kutoka Makanisa mbalimbali nchini na Wasanii wa Muziki wa kizazi ...