Skip to main content

MAKAMU WA RAIS MTEULE AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

#subscribe on youtube "YOHANEC CHANG'A"

Makamu wa Rais Mteule, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akizungumza na watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakati wa kuwaaaga rasmi baada ya kuteuliwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kupitishwa na Bunge kushika wadhifa huo, jijini Dodoma ambapo aliwataka watumishi hao kuendelea kufanyakazi kwa bidii ili kuendeleza utekelezaji wa miradi ya maendeleo.


Na Josephine Majura na Farida Ramadhani, WFM, Dodoma
MAKAMU wa Rais Mteule, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, amekutana na Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango na kuwasisitiza kuendelea kufanya kazi kwa bidii kutokana na umuhimu wa Wizara hiyo katika maendeleo ya nchi.

Mheshimiwa Philip Isdor Mpango, ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Fedha na Mipango, alitoa rai hiyo jijini Dodoma alipokutana na watumishi wa Wizara hiyo katika ofisi zilizopo Treasury Square, akitokea bungeni baada ya kuteuliwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Bunge kuthibitisha uteuzi wake kwa kura za kishindo.

Dkt. Mpango amewataka watumishi wa wizara hiyo kuendelea kufanya kazi kwa weledi kwa kuwa wizara hiyo ni moyo wa Serikali na kwamba wasipofanya kazi vizuri na kwa uaminifu hakuna miradi ya maendeleo itakayotekelezwa, mishahara haitapatikana wala mikopo itakayokopwa hivyo kukwamisha maendeleo ya wananchi.

Alisema hana shaka na uwezo wa viongozi na wataalam wa wizara ya fedha na wengine wanaoshirikiana na na kuwaomba waendeleze ushirikiano kwa viongozi wao waliobaki na Waziri wa Fedha Mpya atakaye teuliwa ili waendelee kuwatumikia watanzania, kama ambavyo walimpa ushirikiano katika kipindi chote alichofanya kazi kama Waziri wa Fedha na Mipango kwa takribani miaka 5 na nusu.

“Taifa hili ni Tajiri na kama nilivyoweka msimamo wangu huko nyuma masuala ya kuombaomba mimi sitaki na naahidi huko ninakokwenda nitalisimimia jambo hilo kwa sasabu ninaamini kwamba Tanzania ina rasilimali nyingi, hatustahili kuombaomba na jeuri yangu ni ninyi!”. Alisisitiza Dkt. Mpango.

Aliongeza kuwa Serikali inawategemea watumishi wa Wizara kuongoza jitihada za Taifa kujitegemea kwa kufanya kazi kwa uzalendo na kutanguliza maslahi ya nchi kwanza ili ndoto ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ya kuwaletea wananchi maendeleo ifikiwe.

Aliwaomba watanzania wamwombee na pia wamwombee Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ili waweze kutekeleza majukumu yao ya kuliletea Taifa hili maendeleo na kutekeleza miradi mikubwa inayoendelea pamoja na miradi mipya itakayoanzishwa lakini pia kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi.

Aliutaka uongozi wa Wizara kusimamia vizuri makusanyo na matumizi ya Serikali ili fedha zinazopatikana ziweze kusaidia kuwaondolea wananchi umasikini kwa sababu kila mtumishi aliyepo Wizara ya fedha anabeba zaidi ya watu milioni 60 mgongoni mwake hivyo kila mtu afanye wajibu wake kwa mama Tanzania.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mwainaidi Ali Khamis, ameahidi kuendelea kushirikiana na watumishi na kumwahidi kuendeleza pale alipoachia na amemtakia majukumu mema huko aendako.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, alimshukuru Makamu wa Rais Mteule, kwa niaba ya Wizara kwa uongozi wake mahili ulioiwezesha Wizara kufanya vizuri katika kusimamia uchumi wa nchi katika kipindi chote cha miaka 5.

Makamu wa Rais Mteule Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ambaye alikuwa Waziri wa Fedha na Mipango amehudumu kwenye nafasi hiyo kuanzia 2015 – 2021 ambapo ameteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na anatarajiwa kuapishwa kesho (31 Machi 2021) saa 9 alasiri Ikulu- Chamwino, Dodoma
Makamu wa Rais Mteule, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akipokelewa na watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango, muda mfupi baada ya kuteuliwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kupitishwa na Bunge kushika wadhifa huo, jijini Dodoma.

Meza kuu ikiongozwa na Makamu wa Rais Mteule, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (katikati), Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwanaidi Ali  Khamis (kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Doto James, wakisalimia na  watumishi wa Wizara hiyo wakati wa kumuaga Dkt. Mpango aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, baada ya kuteuliwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kupitishwa na Bunge kushika wadhifa huo, jijini Dodoma.

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James akitoa neno wakati wa kumuaga aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ambaye sasa ameteuliwa kuwa Makamu wa Rais, jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akitoa neno la shukrani wakati wa kumuaga aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ambaye sasa ameteuliwa kuwa Makamu wa Rais, jijini Dodoma.


Comments

Popular posts from this blog

8 Most Beautiful Brazilian Actresses

#subscribe on youtube "YOHANEC CHANG'A" Na Yohanec Chang'a- Iringa Brazilian women are like the sun: bright, positive, and so dang hot. It’s especially evident when you look at the models, actresses, and other juicy celebs. These women have used their immense sexuality and became the standard of beauty for men around the world. Here are the eight most beautiful Brazilian actresses. 1. Vivianne Pasmanter Vivianne’s parents dreamed that their daughter would do ballet professionally, but the girl did not like that idea and instead wished to become an actress. And she did it. Now Pasmanter can, without exaggeration, be called one of the most famous actresses on Brazilian TV series such as “Nuovo Mundo” and “Alén, Luz de Luna.” 2. Christine Fernandes Although Christine was born in Chicago, Illinois, the future actress returned to her parents’ historical homeland in Brazil at the age of three. She came to the film industry from the modeling business and almost immediately s

HAPPY BIRTHDAY BABA ASKOFU

#subscribe on youtube "YOHANEC CHANG'A" Heri ya kumbukizi ya siku mfanano ya kuzaliwa kwako Mhashamu Askofu Method Kilaini, Askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba. Wapendwa karibuni tuungane na kumtakia heri na matashi mema Baba Askofu Kilaini anapofanya kumbukizi ya siku mfanano ya kuzaliwa.

PETER MSECHU NATAKA NIONGEE NA WEWE KAKA KUHUSU TUNGO ZAKO KWA HAYATI MAGUFULI

#subscribe on youtube "YOHANEC CHANG'A" WAKATI bado tunaomboleza msiba mzito wa Taifa wa kuondokewa na Mpendwa wetu, Aliyekuwa Rais wa Taifa letu la Tanzania, Mpenda Amani, Mpenda watu wake hususani wale wenye hadhi ya chini na kipato kidogo, Mpenda Maendeleo, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Kaka Peter Msechu naomba niongee na wewe kitu katika Tasnia yako ya Muziki... Kiukweli baada ya kutangazwa Kifo cha Hayati Dkt. Magufuli Machi 17, 2021 na Aliyekuwa Makamu wa Rais kipindi hicho, Mama Samia Suluhu Hassan, Wasanii wengi nchini walijitokeza kutunga tungo (Nyimbo) mbalimbali kumuenzi Mpendwa wetu aliyetangulia mbele ya haki. Tumeona tungo nyingi zilizojaa wasifu wakumuenzi Hayati Dkt Magufuli, tungo hizo kutoka kwa Wasanii hao wa Tanzania na Vikundi mbalimbali vya Muziki ziliwavutia watu wengi kutokana na kubeba ujumbe wa kweli kwa Taifa letu. Tumeona vikundi kama Tanzania One Theatre (TOT), Vikundi kutoka Makanisa mbalimbali nchini na Wasanii wa Muziki wa kizazi