#subscribe on youtube "YOHANEC CHANG'A" Tufwate njia ya msalaba, . Tuifuwate, mpaka Kalvario. Tusimamepo, bila haya. Msalaba, Msalaba uponya roho. Sala mbele ya Altare. Ee Mkombozi wangu, ninakuja Leo kufuata njia ile uliyoshika siku ya kufa sadaka yetu. Nimetubu dhambi zangu zote; ninataka kugeuza mwendo wangu, ninaomba kwako niwapatie roho za waumini marehemu waliomo toharani, rehema zote zilozotolewa na kanisa kwa Njia ya Msalaba. Nawe Maria Bikira Mtakatifu, uliyefuata njia ile nyuma ya mwanao Yesu, uniangalie kwa wema, unitie moyo mkuu, nisipende dhambi tena, nikivumilia kàzi na usumbufu na mateso na matukio yatakayonipata. Umekosa nini we Yesu, Kushitakiwa bure kwa Pilato, Wenye kustahili hukumu, Si wewe, si wewe Bwana ni sisi. KITUO CHA KWANZA. Yesu anahukumiwa afe. -Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukuru. -Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako mtakatifu. Pilato anamhukumu Yesu ingawa haoni kosa lake, anawaogopa Wayahudi. Anabembeleza urafiki wa Kaysari. Ee Yesu ...
Comments
Post a Comment