Skip to main content

NCCR-Mageuzi Wamlilia JPM

#subscribe on youtube "YOHANEC CHANG'A"

CHAMA cha NCCR-Mageuzi, kimeeleza kuguswa na kifo cha aliyekuwa Rais Dk. John Magufuli na kuwataka watanzania kusimama pamoja ili kuyaenzi mema aliyoyafanya.

Pia kimesema kina imani na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuliongoza taifa kwani jina lake pekee limejipambanua kuwa ni mleta suluhu.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, James Mbatia , wakati alipofika kutia saini kitabu cha maombolezo ya Hayati Rais Dk. Magufuli, katika Ukumbi wa Karmjee.

“Tukitumia hekima zetu vizuri tukawa na utulivu wa fikra tukasikilizana tutamsaidia sana Rais aliyepo sasa wa sita wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzaniua, mama yetu Samia Suluihu Hasan,”alisema Mbatia.

Aliongeza; “Jina lake ni suluhu na na ataleta suluhu kwa taifa ili tuunganishe yale yote yaliyofanyika tangu enzi za nyerere ambaye alifanya mambo mengi ndani ya nchi yetu hata sasa,”.

Mbatia alisema ameguswa na kifo cha Dk. Magufuli na kwamba yako mambo ambayo alijaliwa na Mwenyezi Mungu, akaumia akayanzisha akiwa zawadi kwa watanzania kuweza kuyafanya ili kuifanya Tanzania kuwa salama na kuwa sehemu nzuri zaidi ya kuishi.

“Ni seme tu buriani Rais Dk. Magufuli, sisi wote hapa duniani tunapita. Kifo ni mtihani na nifumbo la uumbaji kwamba binadamu aliyezaliwa kuna kufariki pia,”alibainisha.

Alisema kwakuwa Hayati Dk. Magufuli alimtumaini na alimwamini mwenyezi Mungu anaamini yale yote mema aliyoyatamani na aliyoyaanzisha basi Mwenyezi Mungu ataweka mkono wake ili kasi hiyo iweze kukamilika.

“Kwa kuwa kwenye wimbo wetu wa taifa tunaamini uwepo wa mwenyezi Mungu na ndiyo maana tunaimba Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania na ndani ya wimbo wetu wa taifa tuna nguzo kuu tatu, nguzo ya hekima nguzo umoja na amani hivyo tunatakiwa kuwa na utilovu wa fikra,”alibainisha.

Alisema yote yatawezekana eendapo watanzania wakiwa na umoja wa kitaifa.

“Tanzania ikiwa ni sehemu ya nchi za maziwa makuu na katiba Bara la Afrika tunahistoria ya kuwa kituo cha ukombozi wa kusini mwa afrika.

Na kanuni ya Mwalimu Nyerere ya aliyoanzisha ya kwamba binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja, basi tuwe ndugu wa pamoja, msiba huu utuunganishe pamoja,”alieleza mwanasiasa huyo.

Alisema siyo rahisi kukubari msiba lakini ufike wakati watanzania wakubari kuwa umetokea .

Mbatia aliambatana na Katibu Mkuu wa NCCR-Magezi , Martha Chiombe.

Hayati Rais Dk. Magufuli alifariki Machi 17 mwaka huu katika Hospitali ya Mzena, Jijini Dar es Salaam kwa maradhi ya moyo na anazikwa leo, Chato mkoani Geita.

MWENYEKITI wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, akitia saini kitabu cha maombolezo cha Hayati Rais Dk. MJohn Magufuli, katika Ukumbi wa Karmjee, Dar es Salaam.

Comments

Popular posts from this blog

8 Most Beautiful Brazilian Actresses

#subscribe on youtube "YOHANEC CHANG'A" Na Yohanec Chang'a- Iringa Brazilian women are like the sun: bright, positive, and so dang hot. It’s especially evident when you look at the models, actresses, and other juicy celebs. These women have used their immense sexuality and became the standard of beauty for men around the world. Here are the eight most beautiful Brazilian actresses. 1. Vivianne Pasmanter Vivianne’s parents dreamed that their daughter would do ballet professionally, but the girl did not like that idea and instead wished to become an actress. And she did it. Now Pasmanter can, without exaggeration, be called one of the most famous actresses on Brazilian TV series such as “Nuovo Mundo” and “Alén, Luz de Luna.” 2. Christine Fernandes Although Christine was born in Chicago, Illinois, the future actress returned to her parents’ historical homeland in Brazil at the age of three. She came to the film industry from the modeling business and almost immediately s...

Mkuu wa Majeshi asimulia neno la mwisho kuambiwa na JPM ‘sijisikii vizuri” (+video)

SHARE TWEET SHARE SHARE COMMENTS Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Mabeyo amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan ataitwa pia Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania na sio Amirat kama ambavyo ilipendekezwa. “Nashukuru Baraza la Kiswahili limerekebisha uendelee kuitwa Amiri Jeshi Mkuu na sio Amirat kama ilivyokuwa inapendekezwa”  Mabeyo Mabeyo ametoa kauli hiyo kwenye Uwanja wa Magufuli Chato leo wakati akitoa salamu kwenye Misa Takatifu ya Mazishi ya Hayati Dr.John Pombe Magufuli. RELATED ITEMS TZA HABARI SHARE TWEET SHARE SHARE COMME

Sala kwa Mama Bikira Maria

#subscribe on youtube "YOHANEC CHANG'A" Sala kwa Mama Bikira Maria. Salamu, Maria, umejaa Neema Bwana yu nawe, umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu, sasa na sasa ya kufa kwetu, Amina. Utuombee kwa mwanao Yesu Kristo. #SalamuMaria #SalaniSilaha