#subscribe on youtube "YOHANEC CHANG'A" MWILI wa Dada wa Kazi, Anitha Mfikwa wa Familia ya Mzee Daudi Mtuwa anayesadikiwa kufariki Dunia Machi 21, 2021 kutokana na mkanyagano wa watu katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kwenye shughuli ya kumuaga Hayati Dkt. Magufuli umeagwa leo nyumbani kwao Kimara na kusafirishwa mkoani Njombe. Akizungumza na Michuzi TV nyumbani hapo wakati wa ibada ya kumuaga marehemu huyo, Mwanafamilia ya Mzee Mtuwa, Emmanuel Mayeji amesema baada ya jitihada za kumtafuta Anitha baadae walitambua mwili wake umehifadhiwa kwenye Chumba cha kuhifadhia Maiti katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Mayeji amesema wamekamilisha taratibu zote za msiba huo na wamesafirisha kuelekea mkoani Njombe kwa taratibu za mazishi za marehemu Anitha, huku akitoa shukrani kwa Viongozi wa Wilaya ya Ubungo, Mkoa na Serikali kwa ujumla kwa jitihada zao kuifariji Familia tangu walipofikwa na msiba huo. “Anitha alikuja kwenye Familia ya Mzee Mtuwa akiwa Mdogo sana, alikuwa mtu
Hii ni blog ambayo inatoa habari mbalimbali juu ya kila kitu ambacho kinaendelea ulimwenguni. ikiwa ni habari za #kitaifa #kimataifa #burudani #michezo #uchumi nk.